Muhidin Issa Michuzi " Uncle " akimlisha keki mmoja wa wafanyakazi wa Michuzi Blog wakati wa kusherehekea miaka 10 ya blog hiyo.
Uongozi na wafanyakazi wa Rweyunga Blog unapenda kumpongeza mmiliki wa Michuzi Blog, Muhidin Issa Michuzi ( Uncle ) pamoja uongozi mzima na wafanyakazi wote wa Michuzi Blog kwa kutimiza miaka kumi ( 10 ) ya kuuhabarisha umma wa Watanzania waishio ndani na nje ya nchi.
Rweyunga Blog inatambua kazi kubwa iliyofanywa kwa miaka kumi sasa na inayoendelea kufanywa na Michuzi Blog katika kuwahabarisha na kuwaburudisha wasomaji wake kila kukicha.
Tunawatakia kila lakheri na mafanikio makubwa zaidi ya hapa mlipofika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni