Kiongozi maarufu wa Venezuela,
Leopoldo Lopez amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 13 na miezi
tisa jela.
Kiongozi huyo amehukumiwa adhabu
hiyo baada ya kutiwa hatiani kwa ghasia za mwaka 2014, ambapo watu 43
wa pande mbili za siasa zinazokinzana walikufa.
Leopoldo Lopez mwenye umri wa miaka
44 alikuwa anashikiliwa kwenye gereza la kijeshi tangu Februari 2014.
Wakati wa kutolewa hukumu hiyo
mapigano yametokea baina ya wafuasi wake na wanaharakati wanaoiunga
mkono serikali nje ya mahakama mjini Caracas.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni