.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 28 Septemba 2015

JOSE MOURINHO AKIRI CHELSEA ITAPOTEZA KOMBE NA KILA MECHI IWAPO HAITOBADILIKA

Kocha Jose Mourinho anayependa majigambo ameamua kumeza kiburi chake na kukiri kuwa kwa mwenendo huu wa Chelsea unaoendelea katika Ligi Kuu ya Uingereza watashindwa kutetea taji lao.

Katika kuonyesha kuwa amechukizwa na matokeo ya timu yake Mourinho amesema alitamani awatoe kuwabadilisha wachezaji sita katika mchezo wao na New Castle ulioshia kwa sare ya bahati ya mabao 2-2.

Kocha Mourinho amesema anakerwa na ufanisi duni wa wachezaji wake kama saba bila ya kuwataja majina na kusema iwapo hali haitobadilika Chelsea si itapoteza kombe bali itapoteza kila mechi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni