Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amewaambia wachezaji wake kuwa hakuna hata mmoja aliyesalama iwapo
timu hiyo itaendelea kufanya vibaya katika msimu huu.
Mourinho amesema kuwa itamlazimu
kuwachezesha wachezaji vijana iwapo wachezaji wa kikosi cha kwanza
hawatobadilika na kurejesha tena makali ya ushindi kwa timu hiyo.
Chelsea ambao ndio mabingwa watetezi
wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa sasa ipo katika nafasi ya 14 ya msimamo
wa ligi hiyo pointi nane nyuma ya vinara Manchester United.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni