Mwanasiasa machachari nchini Afrika
Kusini, Julius Malema ametolewa bungeni baada ya kukataa kufuta
matamshi ya kumtuhumu Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,
kuwa ni muuaji.
Kauli hiyo ya Malema ilimfanya
atolewe bungeni na walinzi wa bunge baada kugoma kutoka nje mwenye
kwa hiyari. Mwezi uliopita Malema alimtuhumu Ramaphosa kuhusika na
mauaji ya watu 34 mwaka 2012.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni