Walimu nchini Kenya wamesema kamwe
hawatotishwa kusitisha mgomo wao unaoendelea na kurejea kazini.
Wakati mgomo ukiingia siku ya nane
hii leo, Tume ya Huduma za Walimu Kenya imesema imewaandikia barua
walimu wakuu 5,000, manaibu wao na walimu waandamizi kwa kushindwa
kufuata maelekezo ya namna ya kushughulikia mgomo huo.
Walimu hao waandamizi wamepewa siku
14, kujibu masula kuhusu nidhamu yao yaliyoelekezwa kwao la sivyo
watimulewe kazi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni