Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka
Duniani FIFA Jerome Valcke amesimamishwa kibarua chake hadi
itakapotangazwa tena na kutokana na tuhuma za rushwa anazohusishwa
nazo.
Taarifa iliyotolewa na FIFA imesema
imekuwa ikifahamu mfululizo wa tuhuma zinazomkabili katibu huyo na
inaendelea na uchunguzi kupitia kamati yake ya maadili.
Shutuma zilizoandikwa na gazeti moja
siku yaAalhamisi zimedai kuwa Velcke amehusika na uuzaji wa tiketi za
kombe la dunia kwa ghalama za juu.
Huo ni mwendelezo wa jinamizi
lililoifika FIFA ambapo hadi sasa maafisa saba wa shirikisho hilo
wapo lupango kwa tuhuma za rushwa, tangu mwezi Mei hali iliyopelekea
Rais wa FIFA Sepp Blatter kutangaza kujiuzulu na kuitisha uchaguzi
mwingine wa FIFA utakaofnyika Februari mwakani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni