.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 18 Septemba 2015

TOTTENHAM, SCHALKE NA BORUSSIA DORTMUND WAANZA KWA USHINDI LIGI YA UROPA

Michuano ya Ligi ya Uropa imeanza rasmi kwa msimu wa 2015-2016 huku ikishudia timu za Tottenham, Schalke na Borussia Dortmund wakianza kwa ushindi.

Tottenham wakiwa nyumbani kwenye dimba la White Hart Lane waliibuka na ushindi wa mabao 3 -1 dhidi ya FK Qarabag, ambapo Heung-min Son alicheka na nyavu mara mbili.
                                                      Heung-min Son akishangilia moja ya bao lake 
Apoel Nicosia wakiwa wenyeji wa Schalke walikubali kichapo cha mabao 3-0, huku Borussia Dortmund wakishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya FK Krasnodar.

Matokeo mengine ya michuano hiyo ni Ajax 2-2 Celtic, Bordeaux 1-1 Liverpool
Fenerbahçe 1-3 Molde na Anderlecht 1-1 Monaco.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni