.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 18 Septemba 2015

KARIBU SHULE ZOTE ZA UMMA NCHINI KENYA, ZINATARAJIWA KUFUNGWA HII LEO

Karibu shule zote za umma nchini Kenya, zinatarajiwa kufungwa hii leo kutokana na mgomo wa wiki tatu wa walimu pamoja na ukosefu wa fedha za kuziendesha shule na kuwa mzigo kwa uongozi wa shule.

Katika mahojiano na wakuu wa shule za umma Kenya, yaliyofanywa na gazeti moja la nchini humo imebainika hata shule zinazotaka kuendelea kuwepo wanafunzi shuleni zinakabiliwa na ugumu kutokana na kukosa fedha za uendeshaji.

Wakati huo huo muda uliotolewa na Tume ya Huduma za Walimu (TSC) kwa walimu kurejea kazini la sivyo wataondolewa katika orodha ya malipo ya mshahara ya mwezi huu unaisha leo, kwa mujibu wa agizo hilo lililotolewa wiki iliyopita.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni