.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 18 Septemba 2015

CROATIA YAFUNGA MIPAKA YAKE SABA KATI YA NANE INAYOPAKANA NA SERBIA KUDHIBITI WAHAMIAJI

Nchi ya Croatia imefunga mipaka yake saba kati ya nane inayopakana na Serbia kutokana na wimbi kubwa la wahamiaji kutoka Syria.

Maafisa wa Zagreb amesema hawana jinsi baada ya wahamiaji 10,000kuingia siku moja tu baada ya Hangari kuweka uzio katika mpaka wake na Serbia.

Wakati huo huo, Slovenia imesema imelizuia kundi la wahamiaji katika treni na itawarudisha nchini Croatia.

Idadi kubwa ya watu inayoelekea kaskazini kutokea Mediterranean imetengeneza mgogoro wa kisiasa kwenye mipaka ya nchi zinazounda Umoja wa Ulaya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni