Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL)
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa
michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya
timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili
kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji
wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya
Dodoma watapambana na Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini
humo.
Kundi B, Polisi Morogoro watacheza
na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza
na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa
watawaribisha Kimondo FC uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua
wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Kundi C, Mbao FC watawakaribisha
Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya
Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC
watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirka mjini Moshi na
Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye uwanja wa Karume
mkoani Mara.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni