Maafisa wa ulinzi wa rais nchini
Burkina Faso wametwaa madaraka ya nchi katika mapinduzi, huku milio
ya risasi ikiripotiwa kusikika katika Jiji la Ouagadougou.
Mtu wa karibu wa aliyekuwa rais wa
nchi hiyo Blaise Compaore ametangazwa kuwa ndiye kiongozi mpya wa
Burkina Faso katika televisheni ya taifa.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
ameshutumu mapinduzi hayo katika taifa hilo ambalo lilikuwa ni koloni
la Ufaransa.
Vikosi vya rais vimewafyatulia
risasi waandamanaji ili kuwasambaza katika Jiji la Ouagadougou na
baadhi yao wamekamatwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni