Mabao mawili ya Anthony Martial na
jingine la Juan Mata jana yaliiwezesha Manchester United kushinda
ugenini kwa mabao 3-2 dhidi ya Southampton katika mchezo mgumu wa
ligi kuu ya Uingereza.
Kwa ushindi huo United imefikisha
pointi 13 na kushika nafasi ya pili nyuma majirani zao Manchester
City ambayo ipo kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi 15, huku West Ham
ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 12.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye
dimba la St Mary's wenyeji Southampton walianza kupachika bao kupitia
kwa Graziano Pelle katika kipindi cha kwanza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni