Basi la Utalii na basi la abiria
lililokuwa limewabeba wanafunzi wageni yamegongana huko Seattle,
katika jimbo la Washington nchini Marekani na kusababisha vifo vya
watu wanne.
Picha za video zinaonyesha basi la
"Ride the Ducks" ambalo ni la kampuni inayotumika
kusafirisha watalii katika miji kadhaa ya Marekani likigonga basi
lingine ubavuni katika daraja.
Waliofariki dunia ni wanafunzi
wageni kutoka kwenye Chuo cha Seattle kaskazini, huku watu kadhaa
wakijeruhiwa.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni