Malcolm Turnbull ameapishwa kuwa
Waziri Mkuu mpya wa Australia, baada ya Tony Abbott kung'olewa
madarakani na chama chake katika kupinga uongozi wake.
Bw. Turnbull, ambaye alikuwa waziri
wa mawasiliano chini ya uongozi wa Bw. Abbott, anakuwa waziri mkuu wa
nne wa Australia tangu mwaka 2013.
Baada ya kula kiapo cha kuanza
kutumikia madaraka hayo mapya Bw. Turnbull alihudhuria kipindi cha
maswali bungeni kama waziri mkuu.
Hapo jana Bw. Abbott alisema
kung'olewa kwake madarakani kulikuwa ni kazi ngumu, lakini ameahidi
kuiheshimu serikali mpya.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni