Watu wapatao elfu 23 wamelazimika
kukimbia nyumba zao kaskazini mwa jimbo la California kutokana na
moto mkubwa wa nyika, siku moja tu baada ya gavana wa jimbo hilo
kutangaza hali ya hatari.
Gavana Jerry Brown amesema moto huo
ambao umeuwa mtu mmoja, umeteketeza na kutishia usalama wa majengo
katika eneo le Napa katika kaunti ya Lake.
Zaidi ya watu 1,300 wamekimbilia
Middletown, kaskazini mwa San Francisco, wakati nyumba zao
zikiteketea kwa moto.
Askari wa zimamoto ambao wameungua
wakati wakizima moto huo wanapatiwa matibabu hospitali.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni