Mchezaji wa Manchester United,
Memphis Depay amekiri kuwa bado anamambo mengi ya kujifunza katika
Kigi Kuu ya Uingereza wakati anaporejea kucheza na timu yake ya
zamani ya PSV Eindhoven kwa mara ya kwanza tangu aondoke, na kusema
hatosita kushangilia akifunga goli.
Depay amekuwa akianza kila mchezo
tangu ajiunge na United kwa kitita cha paundi milioni 25, na kufunga
magoli mawili safi dhidi ya Bruges katika hatua ya kuwaniwa kutinga
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wakati huo huo Kocha Louis van Gaal
ambaye ametumia paundi milioni 300 kwa usajili katika miezi 14 tangu
ajiunge na klabu hiyo amekiri kuwa hadhani kama timu yake ni nzuri
kiasi cha kuletaushindani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni