Mamia ya wafungwa katika gereza moja
la nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) wametoroka gerezani wakati
wimbi la ghasia zilizoibuka likisababisha vifo vya makumi ya watu
nchini humo.
Ghasia hizo zilianza jumamosi baada
ya mwendesha taksi Muislam kuuwawa na kuibua mapigano baina ya
wanamgambo Wakristo na wa kundi la Waislam.
Wapiganaji Kikristo wanaojulikana
kama anti-Balaka wameshambulia gereza siku ya jana na kuwaachilia
huru mamia ya wanajeshi na wanamgambo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni