.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 29 Septemba 2015

MWANAFUNZI WAKIKE WA CHUO KENYA AJIUA BAADA YA KUTISHIWA NA BOIFRENDI MZUNGU

Mwanafunzi wakike wa chuo mzaliwa wa Tanzania, Mercy Bundi amejiuwa nchini Kenya kwa kunywa sumu baada ya kuanzisha mahusiano ya mapenzi kwa njia ya Facebook na raia wa kigeni ambayo yaliishia kuwa ya kumdhalilisha, vipigo na vitisho.

Marehemu Mercy mwenye umri wa miaka 19, ameacha ujumbe uliomtaja raia huyo wa kigeni Marco Ritz, ambaye alimtishia kuwa atamshitaki atasambaza picha zake za utupu alizompiga na kuieleza dunia kuwa yeye ni kahaba.

Katika waraka wake huo Mercy amesema siku alipokutana na raia huyo wa kigeni ndipo maisha yake yalipobadilika na kuwa ya matatizo kutokana na kupingwa, kudhalilishwa pamoja na vitisho jambo liliomfanya afikie uamuzi wa kujiua Septemba 12, mwaka huu.

Marehemu Mercy alianza elimu yake ya msingi Kisii, akajiunga na Shule ya Wasichana ya Nyakach na baadae kuhamia shule ya Sekondari ya Mtakatifu Michael huko Nakuru 2013, mwaka huu alijiunga na Chuo cha Bugema, hadi alipojiua.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni