Mshambuliaji mpya wa Manchester
United Anthony Martial ameendeleza makali yake ya kupachika mabao na
kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa amabao 3-0 dhidi ya Ipswich
Town.
Wayne Rooney alipachika bao lake la
kwanza kwake katika msimu huu kwa michuano ya ndani ya Uingereza,
ambapo naye kinda kiungo Andreas Pereira, akipachika bao kwa mpira wa
adhabu alioupiga kiufundi.
Andreas Pereira, akipachika bao kwa mpira wa
adhabu alioupiga kiufundi.
Chelsea imefanikiwa nayo kukata
tiketi ya kutinga hatua ya nne ya michuano ya Kopmbe la Capital One
baada ya kuichakaza Walsall kwa mabao 4-1. Mabao ya Chelsea
yalipachikwa wavunia na Ramires, Loic Remy, Kenedy pamoja na Pedro.
Ramires akipiga sarakasi kushangilia goli alilofunga.
Matokeo mengine ya Crystal Palace 4
- 1 Charlton, MK Dons 0 - 6 Southampton, Newcastle 0 - 1 Sheff Wed,
Norwich 3 - 0 West Brom, Tottenham 1 - 2 Arsenal, Liverpool 1 - 1
Carlisle lakini Liverpool ikapita kwa mikwaju ya penati 3-2.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni