Timu ya Manchester United inamaliza
wiki hii ikiwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza
tangu kocha wao wa zamani Sir Alex Ferguson ajiuzulu mwaka 2013,
baada ya jana kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sunderland.
Katika mchezo huo Memphis Depay,
Wayne Rooney walifunga magoli yao yao ya kwanza katika Ligi Kuu ya
Uingereza tangu mwezi April na kumaliza ukame wa magoli, huku Juan
Mata naye akicheka na nyavu katika dakika za nyongeza.
Memphis Depay akifunga bao la kwanza kwa Manchester United
Nayo Chelsea ililazimika kuamka
kutoka usingizini baada ya kuduwazwa kwa mabao 2 na New Castle na
kufanikiwa kuyachomoa yote kupitia Willian na Ramires na kumaliza
mechi kwa sare ya mabao 2-2.
Arsenal nao wameibuka na ushindi
mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Leicester City, huku Alexis Sanchez
akipachika mabao matatu peke yake yaani hat-trick, katika mchezo
ambao walitanguliwa kufungwa.
Matokeo mengine ni Tottenham 4-1 Man
City, Liverpool 3-2 Aston Villa, Southampton 3-1 Swansea, Stoke 2-1
Bournemouth na West Ham 2-2 Norwich.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni