Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown
ameambiwa kuwa kunauwezekano wa kutopatiwa ruhusa kutumbuiza nchini
Australia kutokana na rekodi yake ya ugomvi katika mahusiano.
Nyota huyo amepangiwa kufanya ziara
ya muziki nchini Australia mwezi Desemba, na tiketi za shoo zake
zinatarajiwa kuanza kuuzwa kuanzia kesho. Chris anasiku 28 za kupinga
zuio hilo.
Mnamo mwaka 2009, Chris Brown
alikiri kosa la kumpiga mpenzi wake wa zamani nyota wa pop Rihanna,
na alishatembelea Australia mara mbili lakini sasa serikali
inashinikizwa kumzuia.
Idara ya Uhamiaji ya Australia
imetoa notisi ya kuonyesha nia ya kumyima kuingia nchi hiyo Chris
Brown, Waziri wa Uhamiaji Peter Dutton amesema.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni