Timu ya Mercedes imerejea katika
uongozi na kushinda mbio za magari za Langalanga huku dereva Lewis
Hamilton akiendelea kuwa mbabe wa mbio za Japan Grand Prix, kwa
kutetea taji lake.
Timu hiyo imefanya miujiza baada ya
kutofanya vizuri mwishoni mwa wiki iliyopita huko Singapore, ambapo
Hamilton amesawazisha makosa na kumaliza kinara huku Rosberg wa
Mercedes naye akitoka nafasi ya nne na kumaliza nafasi ya pili.
Hata hivyo kwa namna Hamilton
alivyoshinda mbio hizo za Japan Grand Prix, kutaongeza upinzani baina
ya madereva hao wawili wa timu ya Mercedes.
Lewis Hamilton akinywa champagne kwenye kikombe alichotwaa


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni