Marekani imeonekana kukerwa na
mipango ya safari ya rais wa Sudan Omar al-Bashir nchini China, licha
ya kuwepo na hati ya kutaka kukamatwa rais huyo na Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa uhalifu wa kivita katika jimbo la
Dafur.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan
amesema kuwa ras Bashir atasafiri kwenda China kukutana na rais wa
nchi hiyo Xi Jinping na kuhudhuria sherehe ya Septemba 3 ya
maadhimisho ya kushindwa Japan katika vita ya pili ya Dunia.
Akiongea Jijini Washington, Msemaji
wa serikali ya Marekani Mark Toner amewaambia waandishi wa habari
kuwa Marekani bado inaamini rais Bashir hapaswi kukaribishwa
kutembelea taifa lolote hadi hapo atakapofikishwa mahakamani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni