Mwanariadha Mjamaica, Usain Bolt
ameonekana akiwa juu ya chombo cha magurudumu mawili wakati akiwasili
kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow Jijini London, siku chache tu
baada ya kugongwa na chombo kama hicho nchini China.
Usain Bolt aligongwa na chombo hicho
na mpigapicha za video katika michuano ya riadha ya mabingwa wa dunia
iliyomalizika nchini China hata hivyo alikuwa na bahati hakuumia
katika tukio hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni