Sakata kuhusiana na meli ya Norway
inayoshikiliwa katika bandari ya Mombasa nchini Kenya limechukua sura
mpya jana baada ya kubaini silaha 34 aina ya rifle zilizotengenezwa
nchini Marekani.
Kubainika kwa silaha hizo kumekuja
baada ya meli hiyo kukutwa na unga mweupe unaohisiwa kuwa ni dawa za
kulevya ukiwa umefichwa kwenye magari ya Umoja wa Mataifa yaliyokuwa
yanapelekwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mamlaka za Bandari ya Mombasa
zimesema Umoja wa Mataifa haukueleza uwepo wa silaha hizo ama mifumo
ya silaha kwenye magari yake hayo yaliyowasili Kenya kutokea Mumbai.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni