Makundi ambalimbali ya akinamama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, wakimpa zawadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amefanya mazungumzo na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kuitumia vema heshima na nafasi waliopewa akinamama nchini ya kushika nafasi ya makamu wa rais kwa mara ya kwanza, hivyo kuhakikisha wanahamasisha wenzao ili CCM iweze kushinda na wanawake kutwaa heshima hiyo.
Bi. Suluhu amesema hayo alipokuwa akizungumza na akinamama wa UWT mkoani Dodoma ikiwa pamoja na kutaja kipaumbele ambapo kimewekwa kwa akinamama katika ilani mpya ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Alisema atatumia nafasi yake kushawishi akinamama kipata vifaa na mazingira rafiki ya kuendesha kilimo cha kisasa ili waweze kukuza uchumi wao, pia kuwawezesha katika vikundi vya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na kukomesha usumbufu ambao akinamama wafanyabiashara wamekuwa wakibughuziwa na mgambo wa jiji.
Mgombea huyo alisema kupitia vikundi akinamama watawezeshwa na fungu la fedha shilingi milioni hamsini fedha ambazo zitatolewa kila kijiji maalumu kwa ajili ya kuwawezesha akinamama pamoja na vijana ili waweze kukuza mitaji yao. Pamoja na hayo Bi. Suluhu alisema Serikali watakayoiunda itashughulikiwa changamoto anuai wanazokumbana nazo walemavu hasa akinamama ili kuwawezesha na wao katika ushindani. "...Kwa upande wa kilimo nitahakikisha nachochea kidogo kidogo ili wanawake wapate vitu kama pembejeo na vifaa vingine kuwawezesha kuendesha kilimo cha kisasa," alisema.
Alisema ilani ya CCM imetoa kipaumbele kwa huduma za afya hasa huduma za mama na mtoto ikiwa ni kutambua changamoto na matatizo wanayokumbana nayo akinamama eneo hilo. Alisema atadhibiti rushwa na matumizi mabaya ya dawa zinazopelekwa wizara ya afya kuhakikisha zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kudhibiti urasimu.
Aliongeza kuwa baada ya ujenzi wa shule za kata kufanikiwa akiingia madarakani anaongeza nguvu katika ujenzi wa mabweni ya wasichana ili kukabiliana na changamoto ya mimba kwa wanafunzi wasichana ambazo zimekuwa zikichangiwa na wao kutembea umbali mrefu na kupata changamoto njiani.
Aidha aliongeza kuwa ili kuonesha Serikali ya CCM inawajali walimu itaunda chombo maalumu ambacho kitakuwa na kazi ya kushughulikia matatizo ya walimu pamoja na kukiwezesha kuhakikisha kinatimiza majukumu yake kiufasaha.
Aliwaomba akinamama kushirikiana kufanya kampeni na kuhakikisha CCM inashinda hivyo akinamama kupata fursa hiyo waliyopewa na CCM kwa sasa. "...Naombeni tushirikiane wote kufanya kampeni nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka ili kuhakikisha tunashin
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni