Maafisa wa Ufaransa wamesema moto
katika nyumba ya makazi kaskazini mwa Jiji la Paris umeuwa watu nane
wakiwemo watoto wawili.
Moto huo katika wilaya ya 18 katika
Jiji kuu la Paris umetokea leo majira ya asubuhi na ulidhibitiwa na
askari wa zimamoto 100 kuudhibiti.
Manusura wanne ambao miongoni mwao
ni mahututi wamelazwa hospitali na mamlaka za nchi hiyo zinachunguza
chanzo cha moto huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni