Picha za video zimeibuka
zikimuonyesha polisi mmoja Jijini Texas nchini Marekani akimpiga
risasi mwanaume mmoja aliyekuwa amenyanyua mikono juu.
Video hiyo iliyotolewa na chombo cha
habari kimoja huko San Antonio, inamuonyesha Gilbert Flores akiwa nje
ya nyumba mikono yake ikiwa juu huku risasi ikifyatuliwa na kuanguka
ukutani.
Polisi walisema mtu huyo alikuwa na
silaha na jaribio lao la kwanza ilikuwa ni kutaka kumpunguza nguvu
ili wamuweke chini ya ulinzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni