.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 29 Septemba 2015

MTOTO WA MAREHEMU PAUL WALKER KUISHTAKI KAMPUNI YA PORSCHE

Mtoto wa kike wa nyota wa filamu za Fast and the Furious marehemu Paul Walker anatarajia kuishtaki kampuni ya kutengeneza magari ya Porsche kutokana na ajali iliyosababisha kifo cha baba yake.

Walker alikuwa ni abiria katika gari aina ya Porsche lililokuwa likiendeshwa na rafiki yake wakati lilipogonga nguzo na kulipuka moto Novemba mwaka 2013 na kusababisha vifo vyao.

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kufunguliwa shitaka la kifo cha makosa na binti wa Walker aitwae Meadow, kwa madai watengenezaji gari hilo hawakuzingatia usalama wa waendeshaji.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni