Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani
Papa Francis ameliambia Baraza la Congress la Marekani kuwa Marekani
inapaswa kuwaona wahamiaji kama binadamu na si nambari ya watu.
Akiongea katika fursa maalum ya
kuhutubia baraza hilo Papa Francis amesema wahamiaji wanapaswa
kuchukuliwa kwa upendo na uvumilivu ambao watu wote tungependa
kufanyiwa.
Katika hotuba yake Papa Francis
amerejea wito wake wa kutaka kuondolewa kwa adhabu ya kifo, pamoja na
kuwahudumia vyema masikini na makundi yaliyokosa fursa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni