Rais Yoweri Museveni wa Uganda
amesema kitendo cha kupata watoto kwa uzembe na kutegemea wasamaria
wema kuwaangalia kinachangia ongezeko la kuwapo kwa watoto ambao
maisha yao yapo hatarini nchini humo.
Akiongea katika maadhimisho ya kumi
ya kituo cha Watoto cha Kampala (KCC) kinachoangalia watoto
waliohatarini, Rais Museveni ametaka kuwapo kwa nidhamu miongoni mwa
raia wa Uganda ili kuepusha kile alichokiita kosa la kijamii.
Amewaasa watoto wa kituo hicho
kutojitumbukiza katika masuala ya uzazi hadi hapo wakati muafaka
utakapofika, na kuwasisitiza kutofanya ngono zembe jambo ambalo
linaweza kuwafanya wapate maambukizi ya Ukimwi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni