Na Mubelwa Bandio
Ni SIKU YA KAZI hapa Marekani. Ama niseme kuthamini kazi. Ama siku ya wafanyakazi. Lakini vyovyote iwavyo, ni siku ambayo wengi wetu hapa Marekani tunakuwa na "siku ya mapumziko". NDIO, DAY OFF katika kusherehekea SIKU YA KAZI.
Mmmmmhhh!!! Umeona eeee?
Nilishaandika kuhusu kinyumenyume cha Bin-adamu katika kutenda, kunena na kuwaza. Kuwa kwanini tuwazishwe vitu kwa namna nyingine?
Kwanini nchi nyingi Afrika zisherehekee UHURU kwa staili ya gwaride kama la WAKOLONI WALIOTUTAWALA?
Kwanini siku ya wakulima isherehekewe mjini, na wapatao "day off" ni wale wasio wakulima ilhali wakulima hawapati sherehe yoyote siku hiyo?
Ni kwenye muendelezo huu wa KWANINI, najikuta naleta MASWALI YAFUATAYO, ambayo nilitumiwa na rafiki yangu, na si mawazo yangu.
TUMUWAZE BIN'ADAM NA UNAFIKI WA MAWAZO YA KIMATENDO.
Soma kisha uwaze, "bin'adamu anawaza nini kutenda atendayo?" Japo nilitumiwa NICHEKE, lakini yaliniwazisha pia HIVI TUNAWAZA NINI?
Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA
"http://changamotoyetu.blogspot.com/search/label/Waliwaza%20nini%3F%3F"
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni