.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Septemba 2015

ROBERT LEWANDOWSKI AFUNGA MAGOLI MATANO NDANI YA DAKIKA TISA NA KUWEKA REKODI

Robert Lewandowski amefunga magoli matano ndani ya dakika tisa baada ya kuingia akitokea benchi la Bayern Munich katika ushindi ulioweka historia katika Ligi ya Kuu ya Ujerumani, Bundesliga dhidi ya Wolfsburg.

Bayern ilikuwa imelala kwa bao moja kwa bila katika kipindi cha kwanza, kabla ya Lewandowski alipoingia dimbani kuchukua nafasi ya Thiago katika kipindi cha pili na kubadilisha matokeo ya mchezo huo kuwa 5-1.

Dakika sita tu kupita tangu aingie uwanjani  mchezaji huyo raia wa Poland alipachika wavuni bao la kwanza na kuongeza mengine manne na kuweka rekodi ya mabao matano yaliyofungwa haraka na mchezaji mmoja katika historia ya Bundesliga. 
                                                          Robert Lewandowski akipachika bao la tatu
               Kocha Pep Guardiola akishika kichwa asiamini alichofanya Lewandowski

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni