.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 10 Septemba 2015

SERIKALI IMEFUTA HATI MILIKI YA MASHAMBA MAKUBWA MANNE

Serikali imefuta hati miliki ya mashamba makubwa manne, badala yake wananchi wenye uhaba wa ardhi waliojiorodhesha kutokana na migogoro hiyo, watapewa ardhi kwa kupimiwa maeneo yao .

Aidha Mashamba yaliyofutiwa hati miliki hiyo ni Tanzania Plantations Limited, pamoja Shamba la Noors lililopo kijiji cha Laroi na kisima cha mungu huko Oljoro.

Kuchukuliwa kwa mashamba hayo na serikali ni kuondoa mgogoro wa muda mrefu uliokuwa unasababisha mapigano ya mara kwa mara na uvamizi wa mashamba na wananchi hao, kwa kudai ardhi iliyokuwa inamilikiwa na wawekezaji hao bila kuendelezwa.

Akizungumza leo Jijini hapa ,Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema serikali imeamua kufuta miliki ya mashamba hayo, ili kuwapa wananchi waweze kugaiwa kihalali na kupimiwa maeneo yao kwa watu ambao hawana ardhi ambao walianishwa hapo awali.

Ameyataja mashamba yaliyofutiwa hati hizo na Rais ni Tanzania Plantion yenye namba lenye hati NP 305,NP 304 na C.T.No 5189 yenye ukubwa wa ekari 6,396 na ni mali ya serikali na stahili ya mwekezaji huyo ni fidia.

Lakini pia katika ufutaji wa mashamba hayo mwekezaji amebakiziwa shamba lenye namba N.371 ambalo analimiliki kihalali lakini kwamakubaliano na serikali ameamua kutoa heka 100 kwaajili ya
kuwasaidia wananchi wenye uhaba wa ardhi na kilimo katika Halmashauri ya Meru.

Amesema baada ya ubatilishaji wa mashamba ya Tanzania Plantion Ltd pamoja na ardhi aliyoitoa mwekezaji huyo kwa hiari yake Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imepata jumla ya ekari 6176.5na Halmahauru ya Meru ekari 925.

Lukuvi amesema Wananchi zaidi ya 2000 watapata maeneo ya kujenga (makazi) na kilimo lakini alisisitiza kazi hiyo itasimamiwa na timu ya wataalam, iliyoundwa kwaajili ya kusimamia ugawaji wa maeneo hayo kwa wananchi wenye uhaba wa ardhi.

Aidha amesema wiki iliyopita mashamba zaidi ya 7 Wilayani Mvumero yalifutiwa ulimiliki wa ardhi,10 Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na hivi mashamba ya watu wakubwa 10 yaliyopo Kilombero Mkoani Mgogoro yatafutwa hati miliki zake, kwani haiwezekani matajiri kula kuku mjini wakiyatelekeza na wengine kukodisha wananchi wazawa kuyalima huku wananchi hao wakiwa hawana ardhi.

Wakati huo huo serikali imefuta hati miliki za mashamba 48, zilizokuwa zinamilikiwa na wawekezaji wilayani Monduli na kuleta kero ya mara kwa mara kwa wananchi pia kwa mkoa wa Manyara Rais amefuta shamba la Ufyomi Gallapo Estate, lenye ekari 120 ili kufidia wananchi 340 waliohamishwa kupisha Hifadhi ya Tarangire.

Mwisho

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni