.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 9 Septemba 2015

UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA


Meneja wa Nishati na Maji wa Kampuni ya Bia (TBL)Mwanza, Sunday Kidolezi (wa kwanza kulia),wakiwa na waandishi wa habari wakati wakitembelea mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.wa Kwanza kutoka kushoto (mwenye shati jeupe), Ni Meneja wa Kiwanda hicho, Raymond Richmond.
Meneja wa Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmond (mwenye shati jeupe) akiwaonesha waandishi wa habari mtambo unaozalisha nishati ya umeme kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.anaoshuhudia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo,Sunday Kidolezi (mwenye fulana ya mistari).Mwingine ni mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, Daniel Mkate,ambaye ni miongoni mwa  waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho.
Raymond Richmond, Meneja wa kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), mapumba ya mchele,yanayotumika kuzalisha nishati ya umeme wa kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo.
Mwandishi wa habari, Daniel Mkate (kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa  Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi, kuhusu changamoto ya upatikanaji wa mali ghafi hiyo na madhara yake katika kuzalisha nishati na athari za mazingira.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bi (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba kwenye magunia, kabla ya kuingizwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.Hapo ni katika eneo  linalotumika kupakulia shehena ya mapumba hayo ya mchele, kutoka kwa msambazaji.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni