Ndege ya British Airways iliyokuwa
ikielekea Jijini London imelipuka moto kwenye injini katika uwanja wa
ndege wa Las Vegas wakati ikijiandaa kuruka na kulazimika abiria wote
172 waliokuwemo kutoka nje kwa kutumia milango ya dharuza.
Maafisa wa uwanja wa ndege huo wa
Marekani wamesema watu wapatao 13 wamekimbizwa hospitali baada ya
kupata majeraha madogo wakati wa kujinusuru maisha yao, kufuatia moto
huo katika injini ya kushoto ya ndege hiyo aina ya Boeing 777-200.
Picha ya ndege hiyo baada ya zimamoto kufanikiwa kuuzima moto huo


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni