Viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU)
Jijini Brussels wanajipanga kuridhia mpango wa kugawana wahamiaji
120,000 katika bara hilo, licha ya upinzani mkali kutoka kwa
wanachama.
Nchi za Romania, Jamhuri ya Czech
Republic, Slovakia na Hangari zilipiga kura kupinga mgawano wa lazima
wa wahamiaji hao kwa nchi wanachama wa EU.
Mkutano wa hii leo pia utajadili juu
ya kuongeza udhibiti wa mipaka ya mataifa ya Umoja wa Ulaya, na
kuongeza misaada kwa mataifa jirani na Syria ambayo ndiyo
inayozalisha wahamiaji wengi.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni