.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 20 Septemba 2015

VICTOR MOSES NA DIAFRA SAKHO WAIZAMISHA MAN CITY NYUMBANI

Wachezaji wa West Ham Victor Moses na Diafra Sakho wameitibuliwa Manchester City kasi yake ya ushindi wa mfululizo katika Ligi kuu ya Uingereza baada ya kuiduwaza nyumbani kwa mabao 2-1.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Etihad Victor Moses anayeichezea West Ham kwa mkopo alipachika bao la kwanza kwa shuti la umbali wa yadi 20, mnamo dakika ya sita tu ya mchezo.

Bao la pili la West Ham lilipachikwa kimiani na Diafra Sakho, huku bao pekee la Manchester City likipachikiwa kimiani na Kevin De Bruyne likiwa ni bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo.
                Diafra Sakho akimpoteza kipa Hart wa Manchester City na kupachika bao
                                         Victor Moses akiruka juu kufurahi bao lake alilofunga

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni