.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 20 Septemba 2015

BAADA YA KUPATA KIPIGO ARSENE WENGER ATAKA FA IMFUNGIE DIEGO COSTA

Kocha Arsene Wenger amelisihi Shirikisho la Soka la Uingereza kumfungia mechi tatu Diego Costa, na kumshutumu refa Mike Dean kwa kushindwa kumudu mchezo wao ambao mshambuliaji huyo wa Chelsea akichangia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal.

Wenger alikera na kitendo cha Costa kutoadhibiwa na refa baada ya kumzaba kofi Laurent Koscielny na kumsukuma chini kabla ya mapumziko na kulazimika beki wa Arsenal Gabriel kutolewa nje wakati alipokerwa na kitendo cha Costa na kulipiza kwa kumpiga teke la nyuma.

Wenger amekiri kuwa mchezaji wake Gabriel alipaswa kutolewa nje, hata hivyo amemtupia lawama refa kwa kuonyesha udhaifu wa kumuachia Costa kufanya makosa bila kumpa adhabu, na kuongeza kuwa wameshangazwa na kiwango cha refa Mike Dean.
              Beki wa Arsenal Gabriel akizuiliwa asiende kugombana na Diego Costa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni