Agizo la serikali ya Kenya kuzifunga
shule zote kuanzia jumatatu katika muda usiojulikana kufuatia mgomo
wa walimu wa shule za umma nchini humo limeibua malalamiko kutoka kwa
wadau wa elimu.
Shule za binafsi ambazo nazo
zimeagizwa kufungwa licha ya kutoathiriwa na mgomo huo, zimeapa
kutotii agizo hilo la serikali lililotolewa kupitia Wizara ya Elimu
ya Kenya.
Viongozi mbalimbali nchini Kenya
wamesema serikali imekimbilia kuzifunga shule badala ya kutafuta
ufumbuzi wa madai ya nyongeza ya mishahara ya walimu. Chama cha siasa
ODM kimetaka shule kufunguliwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni