Walimu nchini Kenya wameanza mgomo
wao wa kitaifa rasmi hapo jana baada ya chama chao kuridhia mgomo
kuishinikiza serikali kuwalipa mshahara mkubwa kama ilivyoagizwa na
mahakama.
Viongozi wa Chama cha Taifa cha
Walimu Kenya wameonya kuwa watasitisha mgomo iwapo tu mishahara mipya
italipwa kama ilivyoamuriwa na mahakama. Walimu Kenya walianza mgomo
baridi tangu jumatatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni