Wazazi raia wa Uingereza
wameunganishwa na mtoto wao mchanga wa kiume baada ya kumtuhumu
daktari mmoja wa El Salvador kwa kuwabadilishia mtoto wao wa kiume
baada ya kujifungua.
Wazazi hao Richard Cushworth pamoja
na mkewe raia wa Salvador, Mercedes Casanella wamesema walikuwa
wahanga wa tukio la usafirishaji watoto.
Jaji nchini El Salvador aliagiza
kurejeshewa mtoto wao halisi wazazi hao baada ya kufanyika vipimo vya
kubaini vinasaba vya DNA, ikiwa ni miezi minne kupita baada ya
kuzaliwa mtoto huyo.
Daktari huyo aliyekanusha kufanya
kosa lolote, anachunguzwa na mamlaka za EL Salvador.
Mama Cushworth akiwa na mtoto wake halisi baada ya kujifungua



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni