.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Oktoba 2015

BALOZI SEIF AZUNGUMZA NA WANANCHI WA SHEHIA YA KILIMANI KIDOTI JUU YA KERO ZINAZOWAKABILI KWA MUDA MREFU

Mwakilishi wa Wananchi wa Shehia ya Kilimani Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwasilisha changamoto zinazowakabili wananachi wa Kijiji hicho mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani aliyefika kuitika wito waliomuagiza.
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kilimani Kidoti wakisikiliza nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kumueleza changamoto wanazopambana nazo kijijini pao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwaahidi Wananchi wa Kijiji cha Kilimani Kidoti kwamba Serikali Kuu itazingatia changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi inayostahiki. Picha na – OMPR – ZNZ.

                                                                                    Na Othman Khamis Ame, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameahidi kufutilia na hatimae Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutafuta mbinu za kutanzua changamoto zinazowakabili Wananchi wa Shehia ya Kilimani Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema changamoto hizo zikiwemo fidia ya nyumba, mazao, Madrasa pamoja na uvamizi wa eneo la Ardhi zitapatiwa ufumbuzi bila ya kuleta hitilafu kwa upande wowote uliohusika na changamoto hizo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza na Wananchi wa Shehia ya Kilimani Kidoti mara baada ya kupokea kero zinazowakabili ambazo nyengine zina muda mrefu sasa bila ya kupatiwa ufumbuzi Mkutano uliofanyika katika Skuli ya Maandalizi ya Kilimani Kidoto Jimbo la Nungwi.

Alisema Mwananchi wote wa Taifa hili wanahitaji kupata maendeleo katika maeneo wanayoishi kwa vile maendeleo hayo hayana itikadi, kabila, rangi, dini wana sehemu wanayotoka.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalielewa tatizo la Wananchi hao kuhusu fidia za mali na mazao yao kufuatia kupita kwa Bomba ya huduma za maji safi na salama katika Kijiji chao.

Alisema juhudi zitachukuliwa na Serikali Kuu kupitia Wizara ya Fedha kulipa fidia ya mali na mazao ya Wananchi hao kadri hali itakavyoruhusu kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu Wana Kijiji hao hasa wale waliobomolewa nyumba zao.
 

Akizungumzia suala la Maskani ya CCM ya Kijiji hicho iliyohodhiwa na upande wa Upinzani Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi aliwanasihi Wana CCM wa Kijiji hicho kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa Jengo jengine.


Alisema yeye binafsi atakuwa tayari kusaidia nguvu za uwezeshaji wa Vifaa kwa ajili ya ujenzi huo hatua ambayo itaondosha fitna, majungu na mgongano unaoweza kuleta athari hapo baadaye baina yao na wale wa Upinzani walioamuwa kuihodhi maskani yao.

Naye Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi aliwataka Wananchi wa Kijiji hicho kuwa na subra huku akitafuta nguvu za ufadhili ili kuanza kuunga mkono ujenzi wa Madrasa ya Kijiji hicho.

Mama Asha alisema hatua zitachukuliwa katika kutoa vifaa vitakavyoanzia ujenzi huo ili kutekeleza ahadi iliyotolewa kwa Wana Kijiji hao kusaidiwa nguvu za ujenzi huo.

Wakitoa changamoto zinazowakabili baadhi ya Wawakilishi wa Wananchi hao walilalamikia lugha za Ubabe zinazotolewa dhidi yao kutoka kwa baadhi ya Viongozi wanaoteuliwa na Serikali.

Walisema licha ya jitihada wanazoendelea kuchuku za kufuatilia changamoto wanazopambana nazo katika ngazi mbali mbali kuanzia shehia hadi Mkoa lakini bado wamekuwa wakipambana na lugha mbovu zisizostahiki kutolewa na Viongozi hao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni