Alhamisi, 15 Oktoba 2015
WATANZANIA WAHIMIZWA KUMUENZI BABA WA TAIFA KWA KUCHAGUA VIONGOZI WAADILIFU
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (wa tatu kutoka kushoto) akishiriki Ibada kwa ajili ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere iliyosomwa kwenye Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma leo ikiwa ni maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 16 tokea afariki duni mnamo Oktoba 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas ya Jijini London.Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bibi. Anne Makinda na wa mwisho kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa. Picha na: Frank Shija,WHVUM
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma Padre. Chesco Peter Msaga akiongoza Ibada kwa ajili ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere iliyosomwa kwenye Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma leo ikiwa ni maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 16 tokea atangulie mbeleza haki.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa BwJuma Khatib akisoma risala za utii kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa niaba ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma wakati wa sherehe za kilele cha Mbio hizo, anayemfuatia ni Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji, Vijana, Watoto na Wanawake Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Juma Khamis na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni