Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw.
Ban Ki-moon ametaka kuchukuliwa hatua za haraka kusitisha ghasi
hatari zinazosambaa baina ya Israeli na Palestina.
Bw. Ban Ki-moon amewaambia waandishi
wa habari Jijini Jerusalem kwamba bado mamlaka hazijachelewa mno
kuepusha kutokea mgogoro mkubwa.
Bw. Ban ameongelea ghasia hizo baada
ya polisi kusema Mpalestina aliyekuwa akiendesha gari ameligonga kwa
makusudi kundi la Waisrael katika ukanda wa maharibi na kujeruhi
mwanajeshi na raia.
Waisraeli wanane na zaidi ya
Wapalestina 40 wakiwemo waliohusika na matukio ya kushambulia
wameuwawa katika wiki za hivi karibuni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni