Bunge la Nepal limemchagua mwanamke
mwenye kufuata kampeni za mrengo wa kulia Bi. Bidhya Devi Bhandari
kuwa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya taifa hilo.
Bi. Bidhya Devi Bhandari anakuwa
mtu wa pili kushika wadhifa huo wa urais ambao hauna madaraka ya
kiutendaji katika serikali.
Rais huyo mteule mwenye umri wa
miaka 54, kwa sasa makamu mwenyekiti wa chama cha Kikomonist Nepal
cha United Marxist Leninist.
Bi. Bhandari aliwahi kushika wadhifa
wa Waziri wa Ulinzi kutoka mwaka 2009 hadi 2011. Ameahidi kutetea
haki za makundi machache pamoja na wanawake Nepal.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni