Waziri Mkuu mteuli wa Canada Justin
Trudeau amethibitisha kuwa ataziondoa ndege za nchi yake zinazofanya
mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la Dola ya Kiislam (IS) nchini
Irak na Syria.
Bw. Trudeau amemfahamisha rais
Barack Obama juu ya uamuzi huo saa chache baada ya kukiongoza chama
chake cha Liberal kushinda uchaguzi wa wabunge.
Ikiwa ni sehemu ya kampeni zake Bw.
Trudeau aliahidi kuzirejesha nyumbani ndege zao za kivita za CF-18,
ambazo zilipelekwa katika ukanda huo kushambulia IS hadi Machi 2016.
Hata hivyo hajaeleza ataanza kufanya hivyo lini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni