Makamu wa rais wa Marekani Bw. Joe
Biden amesema anaunga mkono operesheni ambayo ilifanikisha kuuwawa
kwa kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden, akionesha kubadili msimamo
wake wa awali.
Bw. Biden anafikiria kugombea urais
wa Marekani na kauli yake ya awali inamfanya kuchukuliwa kama mtu
ambaye anayesita kushambulia, ambapo pia anachukuliwa kama mwanasiasa
mzigo.
Bw. Biden alinukuliwa akipendekeza
rais Obama asifanye shambulizi hilo wakati akiongea na baraza la
Congress mwaka 2012, kwa mujibu wa shirika la habari la ABC. Hata
hivyo jana Bw. Biden amesema alimwambia rais kwa siri aendelee na
mpango wa kumshambulia Osama.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni