Viongozi sita wa kanisa moja kubwa
la nchini Singapore wametiwa hatiani kwa kosa la kujipatiwa kwa njia
za udanganyifu fedha za kanisa zinazofikia kiasi cha dola milioni 50.
Hukumu ya Jaji imesema mchungaji wa
kanisa hilo la City Harvest, Bw. Kong Hee pamoja na wenzake walitumia
fedha za kanisa kumsaidia kimuziki mkewe Sun Ho ambaye ni mwimbaji wa
muziki wa kidunia.
Katika utetezi wao viongozi wa
kanisa hilo wamesema kuwa walitumia fedha hizo kumsaidia kukua
kimuziki Bi. Ho ambaye ni mwanamuziki wa pop ili kuweza kutumia
muziki wake kuwafikia watu wasio waumini wa dini ya kikristo.
Viongozi hao sita wa kanisa waponje
kwa dhamana hadi hapo watakaposomewa adhabu yao, hata hivyo
wanakabiliwa na adhabu ya kifungo jela kinachoweza kuwa cha maisha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni